Utangulizi.
Uwepo wa ukaguzi wa ndani.
Marekebisho ya Sheria ya fedha za umma ya mwaka 2001(Public Finance Act(2001)) sehemu ya ya 3(1) a –b imeanzisha ofisi ya Mkaguzi wa ndani Mkuu wa serikali ambaye amepewa jukumu la kuziongoza na kuzisimamia idara na vitengo vyote vya ukaguzi wa ndani katika taasisi za serikali Tanzania.
Aidha sheria ya fedha za serikali za mitaa namba 9 ya mwaka 1982sehemu ya 48 imeziagiza mamlaka zote za serikali za mitaa Tanzania kuanzisha vitego vya ukaguzi wa ndani .
Ukaguzi wa ndani Tanzania unafuata mwongozo wa ukaguzi wa ndani wa kimataifa na Tanzania ni wanachama wa Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani ya Kimataifa (IIA).Mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali anasimamia utekelezaji wa mwangozo wa Wakaguzi wa Ndani wa Kimataifa (IPPF).
Maana ya ukaguzi wa Ndani.
Kwa mujibu wa mwongozo wa Ukaguzi wa ndani wa Kimataifa (IPPF)Ukaguzi wa ndani ni shughuli huru,yenye lengo maalum la kutoa uhakiki na ushauri unaolenga kuongeza tija na kuboresha utendaji wa Taasisi kwa kuchambua na kuboresha usimamizi wa vihatarishi,kuimarisha udhibiti wa ndani na utawala bora.
JINSI KITENGO KINAVYOFANYA KAZI.
Kitengo kinaandaa mpango kazi wa ukaguzi wa mwaka ambao huwa tayari ifikapo june ya kila mwaka.Mpango kazi huu huonyesha maeneo yatayokaguliwa(Audit Universe) na muda ukaguzi huo utapofanyika.Mpango kazi wa mwaka hugawanywa kwa robo ambapo kila mkaguzi hupangiwa kazi zake na mkuu wa kitengo husimamia ili kuona ubora unapatikana.Mpango kazi wa mwaka hupitishwa na Kamati ya Ukaguzi,Menejimenti na Baraza la Madiwani kabla ya Kuanza kutumika. Wakaguzi huandaa prorammu ya ukaguzi na kufanya vikao vya awali nawakaguliwa(entrance meeting) ambapo dhumuni la ukaguzi huelezewa na Mkaguzi hupata fursa ya kujua shughuli zinavyofanyika pamoja na miongozo na sheria zinazoongoza shughuli hizo.Baada ya kikao hicho Wakaguzi hufanya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali(inhouse review) na ndipo huandaa mpango wa kutekeleza ukaguzi huo.Wateja wetu wakubwa ni wakuu wa idara na vitengo ambapo shughuli husika hafanyika.Kwa kushirikiana na Mkaguliwa ukaguzi hufanyika na taarifa ya awali huandaliwa na kujadiliwa pamoja na mkaguliwa kabla taarifa ya mwisho kuandliwa ikiwa na maoni yamkaguliwa.
TAARIFA ZA UKAGUZI WA NDANI.
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kinatakiwa na kinaandaa taarifa a Ukaguzi kila robo mwaka.Lengo la taarifa hizi ni kuiarifa kamati ya Ukaguzi,Menejimenti na Baraza kazi zilizofanyika ,matokeo ya ukaguzi na makubaliano na jinsi ya kurekebisha maeneo ambayo yanataka kuboreshwa kama yapo.Taarifa za ukaguzi huwasilishwa kwenye kamati ya Ukaguzi,Menejimenti na Baraza la Madiwani kwa kujadiliwa na hatimaye hupelekwa kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali ,Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa na Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali Mkoa.
Kitengo kinafuatilia na kusimamia utekelezaji wa yaliyojiri kwenye taarifa hizo.
Uyui District Council
Anuani ya Posta: S.L.P 610
Simu ya Mezani: +255 26 296 6008
Simu ya Mkononi: (1) +255 768867886
Barua pepe: ded@uyuidc.go.tz
Copyright ©2016 UyuiDC . All rights reserved.